SEHEMU YA PILI: MAHESABU YA IDADI YA MIFUKO YA CEMENT NA MCHANGA INAYO HITAJIKA KUJENGEA NYUMBA YAKO

Habari wana Ujenzi!, tunaendelea na muendelezo wa kufanya mahesabu ya malighafi za ujenzi. Ikumbukwe hapa tuna lenga kupanua maarifa ili kuwa na upana wa ufahamu wa mambo mbalimbali ya ujenzi kama ilivyo lengo la group hili.

Kwahiyo leo tunaingia sehemu nyingine ambayo itahusu ukadiliaji wa idadi ya mifuko ya cement itakayo hitajika kujengea jengo lako

NB: kumbuka haya huwa ni makadilio, hivyo sio lazima yawe exactly asilimia 100, lakini mara nyingi yako karibuna ukweli halisi kwa asilimia kubwa sana

Tukichukulia mfano wa TOFALI 2,000

Hapa nazungumzia tofali ambazo wengi wanaziita za block, ambazo kitaalamu zinaitwa SAND CEMENT BLOCKS

Hapa tuseme idadi ya tofali za msingi (inch 6) ni tofali 700

Idadi ya tofali za kuta (inch 5) ni tofali 1,300

A: IDADI YA MIFUKO YA CEMENT KWAAJILI YA MSINGI (TOFALI INCH 6)

-Ikumbukwe hapa tofali hizi hujengwa kwa kulazwa

-hivyo tofali hizi zitahitaji cement na mchanga zaidi kuliko zile za kusimama (inch 5)

KANUNI

Mfuko 1 wa cement unajenga tofali 45 za msingi (inch 6 - za kulaza)

Hivyo ukichukulia zile tofali 700 za msingi kwenye ule mfano wetu itakuwa ifuatavyo

Tofali 700 gawanya kwa 45 = 15.5 sawa na mifuko 16 ya cement

NB: (ikumbukwe watu wengine hufanya mfuko 1 wa cement unajenga tofali 50 ama 60 za msingi za kulaza) ili kupunguza gharama, lakini inamaanisha ubora unapungua pia.

B: IDADI YA MIFUKO YA CEMENT KWAAJILI YA KUTA (TOFALI ZA INCH 5)

-Tofali hizi mara nyingi hijengwa kwa kusimama

-Hivyo hazili mchanga na cement nyingi kama zile za msingi

KANUNI

Hapa mfuko 1 wa cement unajenga tofali 60 za kuta (inch 5- za kusimama)

Hivyo ukichukulia tofali 1,300 za kuta kwenye ule mfano wetu, itakuwa kama ifuatavyo

Tofali 1,300 gawanya kwa 60 = 21.6 sawa na mifuko 22 ya cement

NB: (ikumbukwe watu wengine hufanya mfuko 1 wa cement unajenga tofali 70 mpaka 90 za kuta, za kusimama)ili kupunguza gharama, lakini inamaanisha ubora unapungua pia.

NB: KIPIMO CHA MCHANGA

Mfuko 1 wa CEMENT una changanywa na NDOO 9 kubwa za MCHANGA

Ama mfuko 1 wa CEMENT unachanganywa na NDOO 18 ndogo za MCHANGA

MAHESABU YA IDADI YA NONDO KWA AJILI YA MSINGI NA LINTA

Kwanza ni lazima utambue kwamba NONDO zina umuhimu gani katika ujenzi wa nyumba yako.

MUINGILIANO WA NONDO NA ZEGE: nondo na zege zinatengeneza muingiliano sahihi kabisa katika ujenzi. Hii inatokana na sababu mbalimbali

  • - Nondo zina tabia zote yaani nguvu katika mgandamizo (compression strength)na nguvu katika uvutano (tension rate)
  • Zege lina nguvu kubwa ya mgandamizo (high compression strength) lakini haina nguvu kubwa ya mvutano (low/poor tension strength). Hivyo tunapo unganisha hivi vitu viwili yaani zege na nondo unapata tabia zote mbili yaani nguvu kubwa katika mgandamizo na mvutano ama mbonyeo

Ikumbukwe kwamba zege hutumika katika ujenzi wa sehemu mbalimbali katika majengo kama vile MSINGI, NGUZO, BIMU, SLABU, NGAZI, LINTA N.K

Kwahiyo sasa tunaweza kutazama umuhimu wa zege lenye nondo (Reinforced Concrete /R.C) katika ujenzi

o Ni imara, haiathiriwi na moto kiurahisi na haishambuliwi na wadudu kama ilivyo kwa mbao.

o Majengo yenye zege imara haya ruhusu maji na unyevu kiurahisi

o Inapunguza gharama za kufanya marekebisho (maintenance) mara kwa mara

o Zege lenye nondo ni rahisi kulitengeneza katika muundo wowote unao hitaji

Sasa baada ya kupata elimu kidogo na mwanga juu ya nondo na zege kwa ujumla sasa twende kwenye hesabu za namna ya kufanya mahesabu ya idadi za nondo katika jengo.

Kama kawaida yetu tutakuwa na mchoro wa msingi utakao tusaidia kufanya mahesabu (utakao tumika kama mfano).

Kwanza ni vizuri kutambua kwamba nondo zipo katika ukubwa mbalimbali

Nondo huanzia ukubwa wa kipenyo cha 8mm, 10mm, 12mm, 16mm, 20mm, 25mm na 32mm. hizi zote huwa na urefu wa 12m. (‘mm’ maana yake milimita, na ‘m’ maana yake mita

Baada ya kujua hilo, ni vema kujua pia kwa majengo ya nyumba za kawaida za kuishi huwa tunatumia sana nondo za 12mm na urefu wa 12m.

KANUNI YA KUTAFUTA IDADI YA NONDO

IDADI= JUMLA YA UREFU WA KUTA (MSINGI) GAWANYA KWA UREFU WA NONDO MOJA KISHA ZIDISHA KWA 4 AU 3

-tunazidisha kwa 4 kwasababu maranyingi nondo hizi huwekwa nne, yaani chini mbili na juu mbili zinafungwa kwenye ring yenye pembe 4

- tunazidisha kwa 3 kwasababu wakati mwingine nondo hizi huwekwa tatu, yaani chinp mbili na juu moja zinafungwa kwenye ring yenye pembe tatu

UKIANGALIA MCHORO WA HAPO JUU JUMLA YA UREFU WA KUTA (MSINGI) NI

4+2+3+4+4+2+4+2+3+4 = 32m (hii ni jumla ya kuta zote za msingi,)

Idadi = (32m/12m)4

=2.66x4

=10.6 sawa na nondo 11

Kwa wanao tumia nondo 3 basi itakuwa

Idadi = (32m/12)3

= 2.66 x 3

= 7.9 sawa na nondo 8

Kumbuka mzunguko wa msingi ni sawa na mzungo wa linta hivyo idadi ya nondo za msingi zitafanana na za linta kama utaweka zote kwa uwiano mmoja.

Ni matumaini yangu muendelezo wa makala hii utakuja uwezo na ujasiri wa kuamua kufanya makadirio ya gharama za kujenga ile nyumba ya ndoto yako.

AHSANTE SANA